Jina lake mwanadada Irene Paul sio geni mno katika fani ya burudani hasa nchini Tanzania Mwanadada huyu ana sifa za kuwa muigizaji hodari , kando na hayo yeye ni mama na mke.

Ni mwanamke aliyeshiriki filamu na vipindi kadhaa na kwa sasa anaonekana kwenye kipindi cha Jua Kali na filamu mbalimbali kwa mfano Love & Power, Kibajaji, Kalunde, Fikra Zangu, Penzi la Giza, I Hate My Birthday na nyinginezo.

Irene anatajwa kama mwanadada anayejua kuzitendea haki nafasi anazopewa kuigiza.Tulipozungumza na Irene hakutaka kukubali kwamba ana umaarufu mkubwa

“Sitaki kusema kuwa nina umaarufu mkubwa , ila ninachoweza kusema ni kuwa kazi zangu zinatambulika mno , hasa kwa kuwa ninafanya kazi na televisheni basi mtu atajulikana kwa haraka kuliko kazi nyingine “anasema Irene.

Uigizaji ambao amefaulu kuufanya kwa filamu za kiTanzania ni kwa kipindi cha miaka 11 Muda huu Irene anasema ameutumia kujitafutia nafasi ambazo zinasongesha taaluma yake hata juu zaidi . Hivi sasa analenga kuimarisha ndoto za wanawake na wasichana katika kanda hii .

Irene Paul , alianza kwa kuwa mtangazaji kwa miaka kadhaa kabla ya kujiunga na uigizaji. Kipindi hiki ni cha tamthilia ambayo mwanadada huyu anaigiza kama mama wa kambo , katika familia yenye baba mzee aliye na watoto ambao mmoja wao ni umri sawia na wa mama wa kambo.

Tamthilia hiyo imelenga sana kuangazia hali zinazofanyika kwenye baadhi ya ndoa barani Afrika ambapo katika ndoa yake Irene anasema kuwa kuna vituko na vitimbi vya kila aina vinavyofanyika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *