Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Kala Jeremiah amesema watu wenye pesa wanaongoza kuharibu mahusiano ya watu kwa sababu changamoto nyingi kwenye jamii inaanzia kwenye ishu za kimahusiano.

Kala anasema wazee wenye pesa wanapokonya wake na wapenzi wa watu, husababisha maumivu, kilio pia husababisha hata mtu kuongea peke yake ambapo ukichunguza chanzo ni mahusiano.

“Watu wenye pesa wanapokonya wake na wapenzi wa watu na hicho ni kitu kibaya na imekuwa kilio na maumivu mengi”

“Changamoto kubwa ya jamii kwa sasa inaanzia kwenye mahusiano, ukikuta mtu kavurugwa anaongea peke yake ukichunguza chanzo chake nyuma ni mahusiano ndio yamesababisha”

Kala Jeremiah ameongeza kusema watu wenye pesa hawaharibu mahusiano au ndoa za watu pkee bali wanaharibu mpaka future za watu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *