Msanii wa muziki wa Rap nchini Tanzania, Rosa Ree amefunguka na kusema kuwa Albam yake imekamilika imebaki kuiachia hivyo amewataka mashabiki wake wakae mkao wa kula kuisubili albam hiyo.
Mwanamuziki huyo amesema kuwa haamini kama albam hiyo imekuwa nzuri zaidi ya alivyotegemea kutokana na ubora wa nyimbo zake kwenye albam hiyo.
Msanii huyo pia amewauliza mashabiki wake kuwa wanataka kumsikia nani akiimba nae kwenye albam yake kati ya marapa wenzake wakike wawili, Frida Amani au Chemical.
Albam hiyo itakuwa albam yake ya kwanza kuachiwa toka aanze muziki huo hivyo amewataka mashabiki wake waendelee kumsapoti kwa albam hiyo.
Rose Ree ni mwanamuziki wa kike wa rap anayefanya vizuri kwenye soka la muziki nchini Tanzania kutokana na ubora wa tungo zake.