Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Darassa ametangaza kusaidia watoto yatima kupitia wimbo wake wa “King of the kings” ambapo asilimia 70 ya mapato yatakayopatikana kupitia wimbo huo yataenda kwa watoto wenye uhitaji na utakuwa ni utaratibu endelevu.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram amepost na kuandika ” Wakati hawa vijana wanatoka kuja kucheza hapa !!! WACHA watu wazima tufanye mambo ya maana.
Leo ninayo furaha kuwatangazia tulianza na nyinyi kama utani, Na tumetokea GIZANI but LookatUsNowCMG we’re officially company.
Lakini wote mnajua tumetokea wapi, Na tutakua watu wa ajabu sana kama tutasahau kumulika huu mwanga wetu kwenye Kiza wako wenzetu kama sisi huko hawaonekani. Na sio kila mmoja anaweza kutoka mwenyewe kwenye shimo la mtaani.
Kwa kutambua hilo na kutambua mchango wa BABA MUNGU wetu kwenye kila hatua, Nimengi ambayo tunapitia kilasiku ni kwa BARAKA zake kua hapa njiani tunaendelea na hii safari.
Mauzo au mapato kutoka digital platforms na chanzo chochote cha kuingiza pesa kupitia wimbo huu 70% zitakwenda kusaidia kwenye vituo vya Watoto wenye uhitaji ( Orphanages ) Hii ni program endelevu lengo ni kusaidia kujenga jamii zetu au kuboresha, Kusaidia watoto watoke mitaani ili tusipoteze nguvu ya kujenga.