Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Oscar Lelo maarufu kama Whozu amefunguka kuwa, amekamatika ile mbaya baada ya hisia zake kimapenzi kutekwa na baby mama wake, Tunda Sebastian.

 

Whozu amesema kuwa, upendo alionao kwa mpenzi wake huyo hauwezi kuelezeka kwani kuna muda anatamani aitie vyombo vya habari na maeksi wake wote awaambie ni jinsi gani alivyo na furaha kwa sasa.

 

“Nashindwa sijui hata niongee kitu gani ila Tunda ananifanya nainjoi sana maisha nikiwa naye kila siku.

 

Huo ndiyo ukweli usiopingika kwamba nimekamatika kwa Mama Lola, huyu mwanamke ananipa ninachotaka,” anasema Whozu ambaye miezi michache iliyopita alifanikiwa kupata mtoto wa kike na Tunda.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *