Filamu ya Slay alioingiza mtanzania, Idris Sultan imefanikiwa kuingia 10 bora ya Netflix nchini Nigeria kutokana na ubora wake.
Imechukua miezi mitatu na wiki kadhaa kabla ya kurejea tena kwa filamu ya Slay aliyoshiriki Mtanzania Idris Sultan kwenye mtandao wa Netflix.
Filamu hiyo ilitolewa kwenye mtandao huo April 26 mwaka huu kwa sababu ya hakimiliki na kufanikiwa kurejeshwa tena August 8. Good news ni kwamba mapokeo yake yamekua makubwa sana.
Filamu hiyo imeingia kwenye Top 10 ya Netflix nchini Nigeria ikishika nafasi ya 5, huku Idris Sultan akiwakilisha vyema Bongo Land kwa kuitendea haki filamu hiyo kwenye maeneo aliyopewa uhusika.