Mwanamuziki wa Hip Hop Bongo, Joh Makini amewataka wasanii wa Bongo Fleva kuacha kulalamika badala yake kufanya kazi kwa bidi ili kupeleka mbele muziki huo.

Joh Makini amesema hayo baada ya baadhi wakisema muziki Unashuka Baadhi Pia Wakisema Bongofleva Ni Kama Inapoteza Uhalisia Wake.

Joh Makini amesema kuwa Ki Upande Wa Biashara Mara Zote Mfanya Biashara Anaanzia Sokoni, Soko La Wasanii Ni Mtaani, Msanii Ni Kioo Cha Jamii Maana Yake Ni Unachokiona Kwa Msanii Amekitoa Mtaani Amekuja Kukiwakilisha.

Pia amesema Msanii Akienda Sehemu Mbalimbali Za Burudani Anakuta Ni Aina Flani Ya Muziki Ndio Inafanya Vizuri Tu Kwa Jicho La Biashara Lazima Msanii Ataona Huo Ni Mtaji Na Lazima Aufanye’.

“Na Zungumzia Kibiashara Mtu Lazima Ataangalia Ni Nini Kinauza Kwasasa Kama Ni Nyanya Zichukue Peleka Sokoni Piga Hela Maisha Mengine Yaendelee.

Hivyo Sioni Tatizo Kwa Baadhi Ya Wasanii Kuamua Kwa Maono Yao Ya Muziki Kuona Sasa Hivi Muziki Flani Ndio Unalipa Wakaamua Kuufanya Kulingana Na Biashara Na Maono Yao Pia Naona Ni Sawa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *