Producer mkongwe wa Bongo Fleva, Master J amesema maudhui ya nyimbo za sasa huwezi kusikiliza ukiwa na wazazi au watoto wako na kuimba kwa pamoja.

Master J ameeleza hayo katika mahojiano yake na Kipindi cha Supa Breakfast cha East Africa Radio akijibu swali aliloulizwa kuhusu maudhui ya nyimbo za sasa, ambapo alisema maudhui yasiyo sawa yanatakiwa yawe na muda maalum ili vijana na watoto wasiyasikilize.

“Kwa mtazamo wangu sio miziki yote maudhui yake yanaridhisha, asilimia mkubwa kama maudhui si mazuri, je utaweza kupiga huo wimbo mbele yao,” amesema Master J

Pia Mastyer J amesema kuwa Baraza la Sanaa la Taifa BASATA halifanyi kazi vizuri mdio maana nyimbo zisizo na maudhui zinapigwa muda wote badala ya kuchujwa ili kupigwa katika muda maalum.

“BASATA hawaifanyi kazi yao vizuri kama wangekuwa wanaifanya, hamna tatizo ila ukishakuwa rated vyombo vya habari vinajua wimbo wako uu-slot wapi na hicho ndicho kinachokosekana, hakuna kuchuja nyimbo, nyimbo zinapigwa kipindi ambacho vijana na watoto wanangali TV,” amesema Master J.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *