Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Ben Pol amesema alitamani kuwahasa watu waliokuwa wakimkejeli kutokana na uamuzi wake wa kwenda mahakama kufungua shauri la talaka.

Kauli ya mwanamuziki huyo inakuja baada ya kuachana na mkewe huyo kutoka nchini Kenya, alisema Watanzania wengi hawajui kwa sheria.

Alisema wanawake ndio waathiriwa wakubwa zaidi kwa sababu talaka yoyote inayotolewa nje ya mahamaka haitambuliki.

“Zile talaka tatu hazina mchongo, chombo chenye mamlaka halali ya kutoa talaka ni mahakama kwa upande wa Tanzania.

Kama mwanamke au mwanaume akisema hii indoa siitaki anaenda kufungua shauri ya talaka mahakamani.“Ile si kuomba talaka, ni kufungua shauri kuwa jamani hii ndoa hainifai tena, na mahakama ndio chombo pekee,” alisema Ben Pol

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *