Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Young Lunya amethibitisha kumshirikisha mwimbaji Mimi Mars kwenye album yake ijayo ambayo ipo mbioni kukamilika.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram anathibitisha kushirikiana na Mimi, akionekana akiwa studio na mwimbaji huyo nyota wa wimbo ‘Wenge’.
Katika post ya Insta Story yake, Lunya pia aliwatag wakali wengine aliokuwa nao, watayrishaji wa muziki ambao pia ni waimbaji, Ammy Wave na Quick Rockar.
Hata hivyo, Lunya anayeandaa ya album yake aliyowashirikisha wakali kibao, alishathibitisha uwepo kwa Emtee wa Afrika Kusini kwenye album hiyo ijayo.