Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Dully Sykes amefunguka na kusema kuwa yeye ndio mwanamuziki wa kutoka nchini Tanzania wimbo wake kuchezwa nchini  Kenya mwaka 2001.

“Mwaka 2001 Mimi Ndio Nilikua Msanii Wa Kwanza Muziki Wangu Kufanya Vizuri Nchini KENYA Nakumbuka Wimbo Wangu Wa Nyambizi Ulifanya Vizuri Sana.

Sasa Mimi Nilienda Kuna Jamaa Alinipeleka Huko (Kwaajili Ya Show) Tukaondoka Watu Watatu Huku Akiwepo Mjomba Wangu, Tumefika Kule Yule Jamaa Akanipa Laki Moja Tu Ama 80k Nadhani, Nilikua Mdogo Sana So Nilikua Sijui Chochote Nimefanya Show Kwenye Uwanja Na Sikua Na Elimu Ambayo Vijana Wanayo Kama Leo (Kuwa Na Management) Kusimamia Suala Kama Hilo Ili Kipato Kiingie Kikubwa”.

”Kwa Kipindi Kile Wao Waliingiza Pesa Nyingi Sana Maana Sikufanya Show Uwanjani Tu Nilipelekwa Na Kwenye Clubs Zingine Bila Kujua Lakini Baada Ya Kupita Miaka Ndio Nilikuja Kujua Kama Jamaa Walinipiga Sikupata Haki Yangu Niliyostahili Kupewa.

Dully amesema kuwa Jamaa Alipewa Hela Nyingi Sana Kwenye Kila Klabu Lakini Yule Jamaa Aliyenipeleka Alichukua Hela Zangu Na Bado Akaja Kuwadanganya Wazazi Wangu Hicho Ndio Kitu Siwezi Kukisahau, Baada Ya Miaka Kadhaa Tulikutana Akiwa Mtu Mzima Sana Tukaongea Na Nikamsamehe”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *