Mkali wa muziki wa Singeli nchini Tanzania, Dulla Makabila ametundika hisia za kuteswa na upweke baada ya mkewe aitwaye Rahima kusafiri nchini Marekani.
Makabila aliweka hisia hizo mtandaoni kupitia akaunti ya Instagram siku chache tangu amuage mke wake huyo aliyeondoka Tanzania kwenda nchini Marekani kibiashara.
Makabila aliyepata umaarufu zaidi na wimbo wake ‘Makabila’ baada ya mahusiano ya muda na Mrembo Rahima waliamua kufunga ndoa Mwezi Mei Mwaka huu.
Tangu wawili hao kufunga ndoa, mbali na kazi za hapa na pale alizokuwa akifanya Makabila, amekuwa karibu zaidi na Rahima hatua aliyoitaja kuwa ni iliyompa furaha zaidi.