Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Dogo Janja amefunguka na kusema kuwa sanaa hususani ya muzikiki inahitaji watu wenye nidhamu la siyo huwezi kufika mbali kisanaa kabisa.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Dogo Janja ameandika kuwa ”Sanaa hua ni uwanja mpana sana.. wala huitaji fimbo au Bunduki kuwashikia watu ili wasikilize mziki wako.

Unahitaji mashairi mazuri yasio na lugha mbaya.. unahitaji instrumental itakayoendana na melody za wimbo husika na mziki unahitaji nidhamu kama kwenye kazi zingine.

Pia ameendelea kuandika kuwa ndio hiki ambacho kimeifikisha hii Album yangu ya pili hapa ilipo ni nidhamu yangu niliyonayo hadi hivi sasa.

Mwisho amemalizia kwa kuandika 1M streams sio jambo dogo kwa mimi.. na ikumbukwe mimi sio mjuzi sana wakutumia ROBOT asanteni wadau wote mnaopenda mziki mzuri.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *