Msanii wa Hip hop kutokea nchini Tanzania, Wakazi amekitetea kingereza cha mkali Diamond Platnumz akiwa na nguli wa Hip hop duniani Snoop Dogg baada ya baadhi ya watu kama kumbeza mitandaoni kutokana na uongeaji wake.
Wakazi wamesema kingereza sio kitu kikubwa sana kwakuwa wapo watu wengi ambao kwao hiyo ni kama lugha ya tatu ama ya pili Kwa kuipa nafasi zaidi.
Kupitia Instagram account yake Wakazi amendika hivi “So alivyojitutumua kusema “I’ma go gerrah” mkamcheka. Sasa hivi kapiga “yes” kama asiyejua, mnacheka tena.
Kiingereza ni lugha tu jamani sio big deal kiivyo. Isitoshe ni lugha ya pili na wengine ni ya Tatu kwao kwa hiyo yupo sawa mana ana lugha yake anayoifahamu vizuri vizuri.
Utumwa wa kifikra ndio unafanya Watu wanakuwa na pressure ya kuongea English ili wa “fit in”. Ila hamna tatizo kabisa kutokijua. Besides, Mtu kama Snoop Dogg anavyokushushia Madini adimu, mlitaka yeye a-INTERJECT?