Mume wa msanii wa Bongo Fleva, Shilole aitwae Rommy 3D amefunguka kuhusu uwezekano wa kuongeza kuoa mke wapili kwa kusema hawezi kufanya hivyo kwa sababu ana mwanamke ambaye yupo full package.

Rommy anasema unapooa mke wa pili ina maana yake mke wa kwanza ana mapungufu japo akiamua kuoa ataoa kwa sababu dini yake ya kiislam inamruhusu hata wanawake wanne.

Rommy amesema kuwa “Nina mwanamke ambaye yupo full package mzuri na mpambanaji, unajua unapooa mke wa pili ina maana mke wa kwanza atakuwa na mapungufu mawili matatu.

Pia amesema kuwa sio kama namuogopa nikiamua kuoa naoa tu watoto wa kiislam sisi tumeruhusiwa hadi wanawake wanne lakini ukimpata anayekamilika huna haja ya kuoa tena.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *