Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Barakah The Prince amesema kwamba wakati anaingia jijini Dar es Salaam kwa mara ya kwanza kutokea Mwanza alitumia usafiri wa ndege na sio gari kama walivyofanya wasanii wengi kutoka mikoani.

Kauli ya Baraka inajiri baada ya Tundaman kumwambia alimsaidia nauli ya kuja Dar es Salaam kwa ajili ya kufanya ishu za kimuziki.

“Mimi sikuja Dar kwa bus nimekuja na ndege mtafute mama Bob Junior ndiye alikuja kunipokea Airport na gari lake, ila Tundaman alinisaidia kunipa Tour yake wakati anafanya show Mwanza, kipindi hicho ana wimbo wake na Spark na hakuna aliyekuwa hatamani kukutana naye” amesema Barakah The Prince

Mengine zaidi aliyoyazungumza Barakah The  Prince kuhusu safari yake ya kufika Dar mtazame hapo chini kwenye video akieleza zaidi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *