Nyota wa Bongo Fleva, Ali ‘Saleh’ Kiba anapomalizia album yake ijayo, ameingia studio kufanya wimbo na mkali za Rap nchini Kenya, khaligraph Jones.
Kiba ambaye yuko Kenya kwa sasa, ameonekana studio kikazi na Khaligraph na taarifa zilizothibitika ni kuwa wawili hao tayari wamerekodi wimbo wa kushirikiana.
Hata hivyo bado haijabainika kama kama Khaligraph ni kati ya watakaoshirikishwa kwenye album hiyo ijayo ya Kiba inayotarajiwa kutoka mwezi Agosti mwaka huu.
Alikiba kwasasa anatamba na nyimbo zake zinazokwenda kwa jina la Ndombolo ambayo amefanya na wanamuziki wa lebo yake King’s Music na Salute ambao amefanya na Rude Boy wa Nigeria.