Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Alikiba amefunguka na kuwataarifu mashabiki wake kuwa kesho ataachia video ya wimbo wake mpya ‘Salute’ aliomshirikisha Rude Boy wa Psquare.
Alikiba amesema kuwa Siku ya kesho Jumatano ndio siku rasmi ambayo video ya ngoma Salute itaachiwa rasmi baada ya kusubiliwa na mashabiki kwa muda mrefu.
Ngoma hiyo imeweka attention kubwa sana mtandaoni kutokana na aina ya wasanii waliopo kwenye ngoma hiyo pia muonekano wa mavazi waliyovaa yakiendana na jina la wimbo ambalo ni Salute yakiwa ya kijeshi.
Video ya ngoma hiyo ya Salute imerekodiwa katika jiji la Lagos nchini Nigeria kipindi ambacho Alikiba alienda Lagos hivyo waliamua kufanya kila kitu kutokana na ratiba za wasanii wote wawili ili kuepusha usumbufu.
Mashabiki wengi wa Alikiba wamekuwa wakisubiria kwa hamu video ya ngoma hiiya Salute kuiona ilivyo na hiyo yte ni kutokana na ukubwa wa wasanii wote wawili.
Ujio wa Alikiba umekuwa wa kitofauti sana kwani ndani ya wiki moja aliachia ngoma mbili moja ikiwa ni NDOMBOLO ambayo ameshirikiana na wasanii wote wa Kings Music.