Wimbo wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Harmonize uitwao Sandakalawe umeondolewa kwenye mtandao wa YouTube kutokana na masuala ya hakimiliki ya wimbo huo.
Taarifa za mtandao huo zimeleeza kuwa kampuni ya usambazaji muziki ‘Empire’ imelalamika kuwa wimbo huo umechukua baadhi ya vionjo kutoka kwao.
Wimbo huo umezuiwa hadi pale pande hizo mbili zitakapokaa na kukubalia. Hivyo kwa sasa mashabiki wa Harmonize nchini Tanzania hawataweza kuusikiliza wimbo huo kupitia YouTube.
Mwaka jana Rosa Ree alimshtaki Harmonize kuchukua mdundo wa wimbo wake ‘Kanyor Aleng’ bila idhini yake na kuutumia katika wimbo wake uitwao Ameen jambo hilo likapelea wimbo huo kufutwa kwenye mtandao wa YouTube kwa kukiuka taratibu za hakimiliki.
Huo ulikuwa ni wimbo wa pili kwa Harmonize kuondolewa YouTube kutokana na mdundo wake kuonekana kunakiliwa kutoka kwenye wimbo fulani, wa kwanza ni Uno ambao Prodyuza wa Kenya, Magix Enga alipeleka malalamiko yake kwenye mtandao huo, kisha wakauondosha kwa muda.
Pia albamu yake, Afro East iliwahi kufutwa kwenye mitandao mikubwa ya kuuza na kusikiliza muziki duniani kama Tidal, Amazon, Deezer, Yandex na YouTube Musi.