Mwanamuziki wa Hip Hop Bongo, Roma Mkatoliki amesema kuwa kabla ya kuanza kusikika na kazi zake kwenye studio ya Tongwe Records alianza kurekodi wimbo wake wa kwanza 2004 Tanga kwa shilingi elfu 70 na uliitwa ‘Masharti ya Mganga’.

Wimbo huo ulirekodiwa katika studio za msanii na mtayarishaji wa muziki  marehemu Abel Motika (Mr. Ebbo) huko mkoani Tanga.

Kwenye wimbo huo Roma aliwashirikisha Kassim na Dickson Msami ambaye aliimba korasi (chorus) katika wimbo huo.

Dickson Msami ambaye kwasasa ni mtangazaji wa East Africa Radio na Tv ndiye aliyempeleka studio za Motika kipindi hicho nakulipia gharama hizo kwa ajili ya kurekodi wimbo licha ya kuwa haukuwahi kutoka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *