Mwanamuziki wa Hip Hop nchini, Moni Centrozone ameipiga kizuizi album yake kwa sharti la kuongeza Subscribers kwenye Chaneli yake ya YouTube.
Moni kupitia ukurasa wake wa Instagram leo Juni 15 2021, aliweka sharti la kuwa ataachia album yake pale atakapofikisha Subscribers 100k kwenye YouTube chaneli yake ambayo kwa sasa ina jumla ya Subscribers 21.9K.
“SITOTOA ALBUM MPK SUBSCRIBER WAFIKE 100k YOUTUBE” Ameandika Moni Centrozone kwenye ukurasa wake wa Instagram.
Moni aliweka kizibo cha msisitizo mzito kwa mashabiki wake ambao hajamfuata kwenye chaneli yake kuwa endapo hatofikia idadi hiyo ya Subscribers album yake hatoachia album na atabaki sikiliza mwenyewe.