Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Anjella amejikusanyia views zaidi ya Milioni 7.97 kwenye mtandao wa YouTube kupitia maudhui (nyimbo) zake zote.
Anjella alijiunga na mtandao wa YouTube mwezi Oktoba 25, 2020 na amekuwa na wastani wa kutengeneza views zaidi ya milioni 1 kila mwezi kupitia kazi zake mbalimbali ambazo amezipakia kwa takribani kipindi cha miezi 7 na nusu hivi.
Ikumbukwe nyota huyo wa muziki wa kizazi kipya wiki iliyopita alikabidhiwa Plaque (Silver Button Award) na mtandao wa Youtube baada ya kufikisha wafuatiliaji (Subscribers) zaidi ya 100,000.
Mafanikio yake hayo ameyapata baada ya kujiunga na lebo ya Konde Gang chini ya mwanamuziki, Harmonize.