Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Amber Lulu amemtetea msanii wa filamu Kajala Masanja kwa kusema haamini kama Kajala anaweza kupiga picha na kuweka pozi kama lile akiwa na mtoto wake Paula Kajala.

“Kiukweli siamini japo vitu vingi vinatokea,yaani kwa mfano mimi na Arianna tukakae kwenye pozi lile ni kitu ambacho hakitawezekana.

Pia amesema kuwa sababu mama yako akikuvulia nguo tu unapata radhi ije kuwa vile kweli? , mtoto akipata tatizo anaeyeumia zaidi ni mama kuliko mtoto” ameeleza Amber Lulu

Wiki iliyopita ili-trend picha isiyokuwa na maadili ambapo ilisemekana ni Kajala na mtoto wake Paula lakini baadaye Kajala mwenyewe alikanusha tuhuma hizo kwa kusema sio yeye bali watu wame-edit picha hiyo kwa lengo la kumchafua.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *