Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Z Anto amesema kuwa ukimya wake wa muda mrefu wa kutoachia kazi, nyuma ya pazia alikuwa anaandaa vitu vya kumrejesha kwa kishindo.
Z Anto amesema kuwa ukimya wake alikuwa chimbo kuandaa albamu mpya yenye nyimbo sita, anayotarajia kuachia wakati wowote kuanzia sasa.
Mwanamuziki huyo amesema kuwa tayari ameishafanya video, kilichobakia wanafanya vikao vya kujadili jina la albamu na kujua wataziachia kwa mashabiki ili wajue kwa nini alikaa kimya.
“Nilikuwa chimbo kuandaa mawe, zitakuwa kazi nzuri maana nimefanya na wasanii tofauti ambao watakuwa sapraizi siku ambayo nitaachia kazi zangu, ambazo nitaziuza sana online kuliko kwa mfumo wa albamu ambao kibiashara ni ngumu kwasasa, kutokana na sayansi na tekinolojia inavyokuwa kwa kasi.
Ameongeza kuwa”Muziki unahitaji ubunifu na kuyasoma mazingira kwa wakati tuliopo,ndio maana nilipata muda wa kujua nahitaji kuipa ujumbe gani jamii, kisha nikaanza kuyafanyia kazi yale niliyoyaona kwamba yanafaa kwa wakati gani.