Muigizaji wa Bongo Movie, Kajala Masanja amevunja ukimya kwa kusema hajafikia hatua ya kukaa mikao isiyokuwa na maadili kama inavyosemekana kwenye baadhi ya picha iliyoeditiwa ikimuonesha yeye na mtoto wake.

Kajala amekanusha hilo kupitia page yake ya Instagram ambapo ametoa taarifa ndefu inayoelezea tukio hilo kwa kuandika kuwa,

“Kumekuwa na picha ikisambaa ikiwaonesha wanawake wawili wakiwa watupu kwenye mkao usiofaa na wanawake hao wameonekana wakitofautiana umri, picha hiyo ikaeditiwa na kuwekwa kichwa changu ama kinachofanana na changu huku watu wakisambaza kwa kusema ni mimi na mwanangu”.

“Hata kama nina ushenzi wa namna gani sijafikia na wala sitafikia huko hiyo ni laana iliyopitiliza sijui waliofanya hivyo wana malengo gani na mimi, sijawahi na sitawahi kupiga picha ya namna hiyo na binti niliyembeba tumboni miezi 9 na kumzaa kwa uchungu”.

Kajala ameamua kusema hayo baada ya muendelezo wa kuzushiwa mambo yasiyofaa katika mitandao ya kijamii kitu ambacho kinamyima sana amani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *