Meneja wa Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, Hamis Tale Tale, amesema harakati za kumpinga msanii huyo kushinda tuzo za mwaka huu za BET hazitafanikiwa.
Wanaompinga msanii huyo kupitia mitandao ya kijamii wanadaiwa kufanya hivyo ili kuonyesha hisia zao kutokana na msanii huyo kushiriki kampeni za Uchaguzi mkuu wa nchi hiyo na kukiunga mkono chama tawala cha CCM, kilichoshinda ushaguzi mkuu wa 2020.
Hamis Tale Tale maarufu kama Babu Tale na ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Morogoro Kusini Mashariki, katika mkoa wa Morogoro, amesema kwamba, wanoendesha kampeni hiyo si mashabiki halisi wa msanii huyo.
‘Hao wanaosema hawatamuunga mkono Diamond si mashabiki wa Diamond na hawajawahi kuwa mashabiki wa Diamond, shabiki hushabikia kile anachokipenda, yaani kufa na kupona’, alisema Tale.
Tale ameonyesha masikitiko kwa wanaaopinga Diamond kwenye tuzo hizo akisema sanaa na siasa ni vitu ambavyo vinaendana. ‘Ni jambo la kusikitisha sana kuona msanii kutoka Afrika, anawakilisha Afrika, ili hali kuna watu ambao wanapiga vita mafanikio ya Afrika’, alisema Karai.
Diamond aliyeshinda tuzo zaidi ya 40 katika mkipindi cha miaka 10 iliyopita ametajwa kuwania tuzo maarufu za mwaka huu za BET katika kipengele cha ‘Best International Act’ akichuana na wasanii wengine maarufu duniani ambao ni Wizkid, Burna Boy, Emicida, Aya Nakamura, Youssoupha, Headie na Young T& Bugsey kutoka Uingereza.