Mwanamuziki wa Hip Hop Bongo, Dogo Janja amefunguka kuwa, hisia za kimapenzi alizonazo kwa mpenzi wake wa sasa, Linah Honnah ‘Queen Linah’ ni kutokana na kukamatika kwake na ndiye mwanamke wa maisha yake.
Janjaro amesema kuwa, upendo alionao kwa mpenzi wake huyo haulezeki kwani kuna muda anatamani hata awapigie simu maeksi wake awaambie jinsi alivyo na fu
Amesema kuwa “Nashindwa niongee nini, lakini ni ukweli usiopingika kwamba sasa hivi nimekamatika, tena nimekamatika haswaa, huyu mwanamke ananipa kila ninachokitaka, heshima.
Pia ameongeza kwa kusema kuwa “Ananipa mapenzi ya dhati na vitu vingine vingi ambavyo sisi wanaume huwa tunavipenda kutoka kwa wapenzi wetu, kiasi kwamba najuta kwa nini sikumjua mapema,”.
Dogo Janja ameingia kwenye mapenzi na mwanamke huyo baada ya kuachana na muigizaji wa Bongo Movie Irene Uwoya.