Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nay wa Mitego amewashukuru wote waliomuombea apone mapema baada ya kupata ajali na kueleza kuwa shukrani zake pia ziwafikie waliomuomzushia kifo.

Mwanamuziki huyo amewashukuru mashabiki wake kutokana na dua walizokuwa wanamfanyia wakati alipopata ajali hiyo ya pikipiki.

Nay ambaye jina lake halisi ni Emmanuel Elibariki alieleza hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram, ambapo kwa sasa anaendelea vyema na matibabu akiwa nyumbani.

Nay wa Mitego anaendelea vyema na matibabu yake baada ya kupata ajali pikipiki usiku wa Ijumaa Mei 28 mwaka huu wakati anawahi kufanyiwa mahojiano na kituo cha runinga nchini.

Nay ambaye alipata ajali akielekea kwenye mahojiano na kituo cha runinga jijini Dar es Salaam na kulazwa katika Hospitali ya Kairuki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *