Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nay wa Mitego amepata ajali mbaya ya pikipiki wakati anawahi kwenye Interview usiku wa jana katika moja yay a kituo cha Tv hapa nchini.
Nay baada ya ajali ulifanyika utararibu kufikishwa katika Hospitali ya Kairuki Mikocheni ambako anapatiwa matibabu ikielezwa kuwa kwa sasa hali yake bado haiko vizuri.
Nay anaelezea kuwa alilazimika kupanda usafiri wa pikipiki ili kuwahi kipindi baada kukwama kwenye foleni akiwa na gari yake.
Msanii huyo bado anapata huduma ya matibabu katika hospitali hiyo kutokana na majeraha aliyoyapata katika ajali hiyo mbaya ya Boda boda.