Mwanamuziki wa Singeli, Dulla Makabila amefunga ndoa na mpenzi wake Rahima anayeishi nchini Marekani akiwafanya biashara zake.
Baada ya kufunga ndoa hiyo Dulla Makabila ameandika “Tarehe 13/06/2020 Siku Ya Birthday Ya Mpenzi Wangu Rahima Nilimuomba Nimuoe Akakubari Ulipofika mwezi Wa 7 Nikatoa barua Kwa Bahati Mbaya Tulipishana Kauli Tukaachana ivyo Zoezi La Kufunga Ndoa Likawa Limekufa Ila Wakati Uo Wazazi Hawakujua Chochte ivyo Ata Barua Haikurudishwa Kila Mtu Alijihisi Amekatiliwa Kuwa Mbali Na Mwenzie Mapenzi Kitu Cha Ajabu Sana Sikuwa Na Rahima ila Nilikuwa Siwezi Siku ipite Siku Nisimfatilie Kapost Nin Wala Nisimpigie Cm Kiukweli Niliteseka Sana Na Sio Mimi tu ata Yeye.
Pia ameandika kuwa Alikuwa Hajiwezi Kila Napomtafuta Alikuwa Anapokea Cm Japo Atanijibu Jeuri ila Aliarijika Kwa Kuona Siwezi Bila Yeye Basi Maisha Yakaendelea Mwisho Nikaona isiwe Tabu Nikampigia Cm Nikamuomba Msamaha Na Nikamuomba Turudiane Kwa Kuwa Kulikuwa Na Mapenzi Kati Yetu Haikuwa Kazi Ngumu Kunielewa Basi Kwa Vile barua Nilishatoa.
Ameendelea kuandika pia Mwezi Wa 4 Mwaka Huu Nikapeleka Mahari Na Process Za Kufunga Ndoa Zikaanza Na Mungu Akajaalia Jana Saa 7 Mchana Nimetimiza Nusu Ya Dini Kwa Kufunga Ndoa Na Mke Wangu Kipenzi Rahima Waziri Furaha Niliyokuwa Nayo Haielezeki Kilahisi Mpaka Muda Huu.
Mwisho amemaliza kwa kuandika kuwa Nahisi kama Ni Ndoto Kwa Upande Wangu Furaha Niliyokuwa Nayo Sio Ya Kuoa tu Bali Ni Ya Kumuoa Mtu Ambae Naempenda Na Yeye Ananipenda Pia Kikubwa Niseme tu Asante Mungu Kwa Kuruhusu Hili Lipite Na Asanteni Ndugu Na Majirani Kwa Kushilikiana Na Mimi Katika Kukamilisha Ndoa Yangu.