Mwanamuziki wa Bongo Movie, Gigy Money amebakiza siku 39 kumaliza kifungo chake cha miezi 6 alichopewa na baada ya Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA).

Basata walimfungia msanii huyo wa Bongo Fleva nchini kutojihusisha na sanaa ndani na nje ya nchi kwa kukiuka maadili ya kazi za sanaa.

Kaimu Katibu Mtendaji wa BASATA, Matiko Mniko,alieleza kuwa wamechukua hatua hiyo baada ya msanii Gigy kutumbuiza jukwaani akiwa amevalia nguo zilizodhalilisha utu wake na kubugudhi hadhira ya wapenda sanaa.

Tukio hilo lilitokea akiwa katika tamasha la muziki huko jijini Dodoma katika uwanja wa Jamhuri na kuamulia kufungiwa kwa msanii huyo.

Gigy Money aliomba kufunguliwa kwa kifungo cha kuomba msamaha kutokana na changamoto za kimaisha alizokutana nazo msanii huyo wakati wa kifungo chake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *