Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Alikiba amefunguka na kuweka wazi kuwa amepata mtoto wa kiume na mke wake Bi. Amina akiwa ni mtoto wa pili katika ndoa ya wawili hao.
Alikiba amethibitisha hayo wakati akifanyiwa mahojiano na chombo kimoja cha habari hapa nchini kuwa amepata mtoto mwingine wa kiume na Bi. Amina ambaye ni raia wa Kenya.
Alikiba amesema kuwa “Unajua wakati mwingine maongezi yana tafsiri tofauti, unavyosikia wewe ni tofauti anavyosikia mwingine unaweza ukamlaumu mtu lakini tumepishana katika uwelewa kila mtu ana uwelewa tofauti.
Pia amesema kuwa unaweza kubishana na mtu mnajibishana kwa kelele kumbe ndiyo uwelewa wake kwa hivyo unapohangaika wote mtaonekana wahangaikaji.
“Kuna watu wanaongea sana kuna maongezi ya faida lakini kuna wengine wanaongea bila faida hawajui chochote”
Pia Alikiba ametoa maana ya jina Sadala lililozua gumzo mitandaoni wiki kadhaa nyuma”Sadala ni jina tu kuna watu wanaitwa Sadala. Mimi kama Mtanzania sikujisikia vizuri sio kulia tu kulalamika katika hali ile lazima kuwepo na kuandikwa katika vitu kama hivyo kwenye Facebook, haijakaa vizuri.
Pia amesema kuwa “Hela ikiwepo huwa unaonekana haiitaji matangazo na ukitangaza watu hawawezi kuamini ukikaa kimya utaonekana na watu wataamini hata debe ukilijaza mahindi ukilipiga halitoi sauti lakini likiwa tupu ukipiga linakwenda mpaka kule. Halafu Sadala wako wengi”.