Mkali wa ngoma ‘Do Lemi Go’ Kinata Mc ameweka wazi kuwa wimbo wake huo aliuandika miaka 2 nyuma ila alikuwa hajapata njia rahisi ambayo angeitumia ili kueleweka sokoni pindi angeiachia rasmi kutokana na uchanga wake.
Wimbo huo ameshirikiana na Ibraah kutoka Konde Music Worldwide ulianza kupata umaarufu kupitia kipande cha video kwenye mitandao ya kijamii.
Wimbo huo umeendelea kutengeneza rekodi mpya kwake kwani mpaka sasa unashika namba 3 kwenye Trending for music huko YouTube.
Kinata ameonesha uwezo wa kuimba kwa lugha ya kiingereza na kiswahili kwenye mdundo wa singeli kwa lengo la kutanua wigo wa soko lake.