Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Mwana FA ambaye kwasasa ni Mbunge amefunguka na kusema kuwa ajawahi kufungiwa wimbo wowote toka aanze muziki ndani ya 19 hadi sasa.
Mwana FA amesema kuwa “Nimefanya muziki kwa miaka 19 na kitu, wimbo wangu hata mmoja haujawahi kufungiwa. Kulikuwa na discpline ambayo mimi ninayo.
Amesema kuwa Lakini kweli sasa hivi muziki ambao mwepesi, una lugha lugha flani ndio unapigwa sana. Kweli kamstari ni kembamba mno, tunataka muziki wetu uende, lakini vipi kuhusu watoto wetu? Tunaweza kusikiliza nyimbo hizi na wazee wetu.
Pia amefunguka Kuhusu Kuonekana Kimya Kiasi Bungeni Wakati Wananchi Wengi Wamekuwa Wakimfahamu Kama Mtu Ambaye Anapenda Kuhoji Mambo, FA amesema Hajazuiwa Kuikosoa Serikali Isipokuwa Kama Mgeni Lazima Ujue Tamaduni Kwanza Ili Usitoe Maboko (Usikosee).
Hatujazuiwa kuikosoa Serikali, hatujaelekezwa hivyo, tena ukweli ni kwamba tumeelekezwa kinyume chake. Tumeelekezwa kuikosoa Serikali, tunatakiwa kuinyoosha na kuielekeza kwa sababu sisi ni wawakilishi wa wananchi. Kuna utaratibu, mimi pamoja na kuwa critic napenda kufuata utaratibu, nisingependa kuwa lopolopo.”