Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Dogo Janja ametangaza rasmi jina la album yake mpya, inaitwa Asante Mama na itatoka kesho Mei 21 mwaka huu.
Kwenye album hiyo kutakuwa na midundo 11 ambayo itasindikizwa na sauti za Wanawake pekee ambao ndio wamepata nafasi ya kushirikishwa.
Kusindikiza album hiyo ya pili, Dogo Janja ametudokeza kuwa mwaka huu ametimiza miaka 10 kwenye kiwanda cha Muziki ambapo Januari 2011 aliachia wimbo wake wa kwanza.
Discography yake imenyooka kwani ametujuza pia katika kipindi chote amefanikiwa kuachia album 1, nyimbo alizorekodi ni 421 na amefanya jumla ya shows 1,562.