Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Dayna Nyange amefunguka na kusema kuwa alitaka kuwa na rangi nyeupe hali iliyomfanya kuanza kutumia madawa ya kubadili ngozi ambayo alitumia kwa muda wa mwaka mmoja.
Dayna Nyange aliyetamba na wimbo wake Mafungu ya Nyanya amesema hayo baada ya kuulizwa kwani ameamua kujichubua mwili wake tofauti na hapo awali.
“Nilipitia situation hiyo ya kutaka kubadili mwili kuwa mweupe kwa sababu mazingira fulani yalitengenezwa kufikia huko na sio kwamba ilikuwa akili yangu kusema nikatafute mafuta ili niwe hivi”.
Amesema kuwa “Asilimia ya watoto wa kike hatuwezi kukaa na kitu kimoja, hiyo ilichangia kuelekezwa mafuta ya kwenda kununua na kuanza kupaka, yakaanza kuning’aza kidogo kumbe unatakiwa ukipaka unatulia baada ya wiki mbili, mimi nikatengeneza hadi pipa natumbukia kabisa, nikatoka muarabu mtoto wa Morogoro”.