Muigizaji wa Bongo Movie, Nisha Bebe amesema kuwa anatamani kuolewa na Ommy Dimpoz baada ya kwenda kuhiji katika mji wa Mecca nchini Saudi Arabia.
Nisha Bebe amesema kuwa Ommy Dimpoz amefanya kitu kikubwa sana na amemshawishi na yeye kwenda kufanya tukio hilo la kuhiji Mjini Mecca, Saudi Arabia kama alivyokuwa anafanya marehemu Mzee Majuto.
Nisha Bebe amesema Ommy Dimpoz amefanya kitu kikubwa sana na amemshawishi na yeye kwenda kufanya tukio hilo la kuhiji Mjini Mecca, Saudi Arabia kama alivyokuwa anafanya marehemu Mzee Majuto.
“Yaani sijawahi kuona picha ya mtu nikatamani kuolewa naye, mara baada tu ya kuiona hii picha nimetamani kuolewa na Ommy Dimpoz na ni kitu ambacho hata akilini mwangu hakikuwepo,umefanya kitu kikubwa sana”
“Serious wa kwanza kunishawishi kutamani kuhiji ni marehemu baba yangu Mzee Majuto, Ommy leo umenikumbusha vitu vingi sana, kiukweli nimejiskia raha kutoka moyoni kwa hiki ulichofanya” ameongeza
Pia amemtaka Ommy Dimpoz asirudie makosa aliyowahi kuyafanya na aendelee kuishi kwenye mstari ulionyooka mpaka mwisho wa maisha yake.