Mwanamuziki wa Taarab nchini, Isha Mashauzi amesema kitendo cha kuvunjika kwa ndoa yao amekitafsiri kama haikua riziki yake kwa sababu alimpenda sana mume pamoja na mtoto wake.
Isha Mashauzi amesema alikutana na mume wake huyo huko Zanzibar baada ya kufukuzwa nyumbani kwao na mama yake mzazi
Ameongeza kwa kusema kuwa “Nilifukuzwa nyumbani na mama baada ya kukutwa na rafiki yangu aliyekuwa amelewa,nikaenda kuishi Zanzibar, huko nilimpata baba mtoto wangu na baada ya hapo ndiyo ikabidi nirudi nyumbani tena kwa ajili ya ndoa, ngawa ndoa haikua riziki”
Pia amesema kuwa “Nilivyoolewa ndoa ya pili, nilikuwa nampenda sana mtoto wa mume wangu na mpaka sasa hivi ameolewa, nilimlea kwa misingi niliyofundishwa mimi” ameeleza Isha Mashauzi.