Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Shilole amefunguka na kusema kuwa sanaa inatakiwa iwe huru na ikichunguzwa sana na wadau wa Sanaa hiyo itaangusha muziki.
Shilole amesema kuwa Sanaa ili ikuwe inahitaji iwe huru zaidi, sio kama naungana na muziki wenye lugha ya matusi hapana ila kila Media ina kitengo cha muziki kama wanajua wimbo fulani una matusi wanajua haifai kupigwa hewani kwa hiyo tuwaachie kitengo cha muziki suala hilo.
“BASATA wakisema waingie ndani kuchunguza nyimbo zetu basi tutauangusha kabisa muziki wetu, wanawezaje kuhakikisha kila wimbo wa msanii kwa kila siku, hata wakina Chris Brown, Rihanna na Wiz Khalifa nazo wanazihakiki kabla ya kupigwa redioni maana wanaimba sana matusi”.
“Mimi naona kutakuwa na ukandamizaji wa sanaa watu wa BASATA wasipoangalia muziki wetu utakufa kabisa natetea hoja yangu kwamba waliangalie upya suala hili ila na sisi wasanii tuongeze ubunifu tuimbe nyimbo nzuri zenye tungo zisizo na matusi, Basata wajiangalie vizuri la sivyo wataua soko la muziki”.