Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Lulu Diva ameshea neno ambalo mama yake mzazi ambalo hupenda kumwambia kila wakati wakiwa wanaendelea kwenye mazungumzo yao.

Lulu Diva amesema mama yake huwa anapenda kumwambia asikate tamaa, apambane, na aongezee bidii kwenye kazi pia kauli nyingine anayopenda kumwambia ni asifananishe kifo na usingizi kwa sababu ni vitu viwili tofauti.

“Mama yangu anatoa sapoti kubwa sana japo hawezi kufanya vitu vingi kwa sababu sasa hivi ni mgonjwa, anapenda kuniambia nisikate tamaa, nifanye kazi kwa bidii, na nipambane halafu ana neno lake moja ambalo anapenda kuniambia kwamba nisifananishe kifo na usingizi”.

Kuna mtu ambaye amezaliwa anacho halafu mimi mtoto wa kimaskini sijazaliwa nacho kwa hiyo lazima upambane na kufanya njia yoyote ili uweze kufanikiwa, naamini katika kufanya kazi” ameongeza Lulu Diva

Tayari msanii huyo ameachia kazi yake mpya ya Mama ambayo inaenda kwa kina mama wote duniani ambao wanapambana katika maisha yako.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *