Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Mwana FA amelitolea uvivu Baraza la Sanaa la Taifa – BASATA kwa mienendo yake ya kuzifungia kazi za wasanii.
Kupitia ukurasa wake wa instagram jioni hii, FA ameandika andiko refu akiwanyooshea kidole BASATA na utaratibu wao huu ambao ameulaani kwa kusema hauna tija yoyote, haumsaidii msanii kwa namna yoyote na ni wa kidwanzi.
Mwana FA ambaye aliwahi kuwa Mjumbe wa bodi kwenye Baraza hilo, amewaomba kutafuta namna nyingine ya kuficha maneno yasiyofaa kwenye Nyimbo za wasanii (Censor) na sio kufungia nyimbo au kutengeneza urasimu kwenye mchakato wa msanii kutoa wimbo kwani ni kuzorotesha sanaa.
Aidha amefilikisha kwa Waziri husika pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara na amesema tumaini lake ni kwamba watalifanyia kazi.