Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Harmonize amechora Tattoo ya aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano nchini Tanzania Hayati John Pombe Magufuli aliyefariki dunia MArch 17,2021.

Harmonize amechira Tattoo hiyo mguuni kwake ambapo ameambatanisha na maneno ambayo Hayati Magufuli alikuwa akipenda sana kuyatumia, “Nime Sacrifice Maisha yangu kwaajili ya Watanzania Masikini”

Harmonize ni kati ya wasanii pendwa wa Hayati Magufuli ambapo pia alishiriki kikamilifu kama msanii kutumbuiza kwenye Kampeni za kumuingiza Madarakani.

Tattoo hiyo ameichora kwenye mguu wake wa kulia akiwa Lagos nchini Nigeria, kisha ameandika maneno yafuatayo “Mimi nime-sacrifice maisha yangu kwa ajili ya watanzania maskini”.

Picha na video hizo akiwa anachora tattoo hizo amezishea kwenye ‘Insta Story’ ya ukurasa wake wa Instagram halafu mwisho wa picha hizo akaandika ‘RIP Kamanda’.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *