Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Ben Pol amethibitisha kuwa kwenye mchakato wa kutalikiana na mkewe Anerlisa Muigai, mchakato ambao unaendelea kwenye mahakama ya Mwanzo Jijini Dar Es Salaam.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Ben Pol kupitia menejimenti yake ametoa taarifa hiyo nakusema Mahakama bado haijatoa talaka wala maamuzi yoyote mpaka pale shauri litakaposikilizwa na kukamilishwa. Pia ameomba nafasi ya faragha (privacy) kwa watu kuacha kuingilia na kuihusisha familia yake katika kipindi hiki kigumu.

TAARIFA: SHAURI LA TALAKA
Ben Pol angependa kuthibitisha uwepo wa shauri la talaka dhidi ya mke wake linaloendelea katika Mahakama ya mwanzo hapa Dar es salaam.

Mahakama bado HAIJATOA talaka/ maamuzi yoyote mpaka pale litakaposikilizwa na kukamilishwa.

Masuala haya ni ya BINAFSI sana na kwa kuwa shauri linaendelea Mahakamani Ben Pol asingependa lizungumzwe zaidi kwa heshima ya pande zote na kwa kuheshimu kazi ya Mahakama.

Pia anaomba nafasi na faragha kwake na kwa familia katika kipindi hiki kigumu. Anawashukuru wote kwa uelewa na pia kwa familia, marafiki na mashabiki wote kwa support mnayoendelea kuionesha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *