Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Dogo Janja ametangaza kuachia album yake mpya ikiwa ni ya pili ambayo ameiandaa kwa muda wa mwaka mzima.
Kupitia Instagram katika taarifa ya ujio huo aliongeza kuwa album yake hiyo atakayotoka rasmi Mei 1 amewashirikisha wasanii wa muziki wa kike tu.
Janja aliweka wazi kuwa album hiyo itakuwa na nyimbo 11 na kuongeza kuwa amewashirikisha wasanii wa kike ni kuonesha ulimwengu uwezo wao ulivyo mkubwa.
Album hiyo ya pili kwa Janjaro ni kuwashirikisha wasanii wa Kike tu, amesema ameamua kuwashirikisha Wanawake tu kwenye album yake ili kuionesha dunia kwamba Wanawake wanaweza.
Na itakuwa na jumla ya nyimbo 11 na wiki ijayo ametaja kuachia orodha ya nyimbo hizo, cover pamoja na jina la album na kudai ametumia mwaka mmoja na siku 21 kuiandaa album hii.