Kampuni ya Naijaonenetflix imeshambuliwa vikali na mashabiki wa Idriss Sultan kwa kumpa uraia wa Kenya na hivyo kupelekea kuishusha Post ya Trailer ya Slya ambayo waliipandisha katika page yao ya Instagram.
Hii ni baada ya Star huyo kuwaomba mashabiki zake kwenda kuwakumbusha kuwa yeye si raia wa Kenya bali ni Tanzania.
Hivyo baada ya Staa huyo kufikia uamuzi huo, baada ya dakika 17 kampuni hiyo imeweza kurekebisha uraia wa Idriss Sultan katika post yao.
Kutokana na ukosaji huo kutoka kwa mashabiki wa Idriss Sultan wameifuta na kupandisha tena mpya ambayo imeelezea Rasmi kuwa Idriss Sultan ni Mtanzania.