Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Madee amesema kuwa kusheherekea siku yake ya kuzaliwa kwa kutembelea gereza Keko kutoa msaada na kuwaona wagonjwa wa saratani hosopitali ya Aga Khan.

Madee ambaye jina lake halisi ni Ahmadi Ali, ameyasema hayo leo kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa Intagram.

Msanii huyo ambaye alikuwa moja ya wasanii waliounda kundi la Tiptop Connection, ameandika”Bado nitaendelea na utaratibu wangu ule ule wa mwaka jana.. sipo tayari kusherehekea siku yangu ya kuzaliwa, bali siku ya leo ntaitumia kuzidisha maombi ili Allah anipe mwisho mema.

“Nitapita sehemu tofauti tofauti kutoa sadaka ya kidogo changu nlichojaaliwa,tutaanzia magereza Keko,kupiga story na wana na kuwakumbusha kuwa wamtumainie Mungu kuna siku na wao watakua nje ya hizo kuta.

“Nitapita Aga Khan hospital kuwapa moyo wagonjwa haswa haswa wa saratani kwa kuwa  ni ugonjwa uliopoteza marafiki zangu wengi sana, ntawapa moyo nakuwakumbusha Mungu ana kusudio lake yeye kuwa hapo na ipo siku ataendelea na shughuli zake kama zamani zaidi wamtumainie yeye,”amesema Madee.

Kama haitoshi mkali huyo wa vibao kama Kazi Yake Mola,Pombe yangu ,Tema Mate, amesema baada ya kufanya hayo atafuturu na washkaji zake katika  kituo cha Manzese hope na kuwawarehemu wote waliotangulia mbele ya haki hukuwa akiwataka watu kuweka majina la marehemu wao ili na yeye awe sehemu ya maombi hayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *