Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz ameonesha kiasi cha mapato aliyoingiza kupitia video ya wimbo wake Waah! aliomshirikisha mkongwe wa muziki Barani Afrika, Koffi Olomide tangu ulipoiachia YouTube, Nov. 30 2020.

Diamond kwa picha zilizoonesha vielelezo vya mapato kwenye mtandao wa YouTube ilionesha kuwa video ya wimbo huo iliyotazamwa zaidi ya mara milioni 60 imemuingizia zaidi ya milioni 89 tangu ilipoiachia rasmi.

Vile vile Diamod alitoa maelelezo juu ya mauzo ya kazi za wasanii na namna kipato kinavyoweza kuwa kikubwa kwa msanii kupitia mauzo ya kazi mtandaoni kama Somo kwa wasio na ufahamu juu ya biashara hiyo ya mtandoani.

Baada ya kuweka wazi mapato hayo, Diamond pia kwa Screenshot ya video ya wimbo Baikoko alioshirikishwa na Mboso alieleza maana ya kuvuma(trending) kwa kazi ya msanii iliyochapishwa kwenye hadhara ya mtandao huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *