Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Lulu Diva amekanusha kutoka kimapenzi na mwanamuziki mwenzake wa Bongo Fleva, Ben Pol baada taarifa za wawili hao kusambaa mitandao ya kijamii.

Kupitia akaunti yake ya Instagram mwanamuziki huyo ameandika “Hata Uongo ukiunyamanzia sana hugeuka kuwa kweli, Nimeshuhudia watu wengi sana wakibeba mizigo isiyokuwa ya kwao na kupakazwa sifa mbaya kwa kukaa kimya tu, Kwangu haitakuwa hivyo tena, Nimeamua kuongea, na huu ndio UKWELI WANGU haijalishi wengine watauchukuliaje

Hapa Juzijuzi kupitia Kipindi cha kina Soudy walinihoji kuhusu Ben Pol, na zaidi wakaipotray kama ni mtu ambae niko nae kwenye mahusiano, nilifanya Interview ile kwa heshima tu niliyonayo juu yao, lakini sasa isigeuzwe habari, Sina mahusiano na BenPol, Sijawahi kuwa na Mahusiano na BenPol, na hiyo habari SIO YA KWELI, na nimesikitika sana kwa jinsi inavyoendelea kuaminishwa kwa watu kupitia MITANDAO, Narudia tena SINA MAHUSIANO NA HUYO KAKA, Na nisingependa nihusishwe kwenye mahusiano nae, namuheshimu kama msanii mwenzangu, na hakuna zaidi ya hapo

Nafahamu kwamba sijawahi kuweka mahusiano yangu wazi, na kuna wengi wanatamani kujua mahusiano yangu, lakini kutoweka wazi isiwe sababu ya kupachikwa na kila mwanaume tu.

Haya ni maisha niliyoyaamua tu kuwa Private na mahusiano, sasa isichukuliwe hii kama fimbo ya kunichapia, maana leo utasikia huyu kesho yule, sitaki, nimechoka na hii tabia, na hata waandishi natamani sana mnapohoji msije na majibu yenu, na wala kuonesha taswira ya namna fulani ya kupotosha, hii inatuharibia wengi, kumbukeni sisi ni Binaadamu na tuna Maisha nje ya muziki, na zaidi tuna familia na tuna future tunayoijenga leo ambayo kama kuna vitu vya kipuuzi itaathiri kesho yetu, hivyo sio kila upuuzi tubebeshwe tu, mi nimegoma kuubeba huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *