Taarifa zilizosambaa leo zinasema kuwa muigizaji wa Bongo Movie, Kajala Masanja na mtoto wake Paula wamekamatwa na Polisi usiku wa jana ikiwa ni masaa kadhaa yamepita toka watue nchini kutokea Dubai.
Inasemekana kuwa sababu ya kukamatwa kwao ni kutokana na sakata la kusambaa kwa video chafu zinazosemekana kuwa ni za staa wa muziki Harmonize.
Taarifa hiyo imesambaza na moja kati ya watu wa karibu na Harmonize H Baba ambaye alipost video fupi ikimuonesha mwanamke akipanda kwenye gari la Polisi na kuandika ujumbe huu.
“Tayari uko wamekamatwa kei na pii jamani jamani Rei umewasababishia wenzio matatizo na post zako ila mngeyamaliza sio poa hili sipendi matatizo pia tusiombeane matatizo usiombe yakakukuta.