Msanii wa muziki wa dansi nchini Tanzania, Muumini Mwinjuma amenasa mikononi mwa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), kutokana na wimbo wake wa Kwa Mpalange aliouachia hivi karibuni.

Muumini aliitwa Aprili 15, 2021 ambapo aliitikia wito na kufika katika ofisi za baraza hilo zilizopo maeneo ya Ilala Sharif Shamba jijini Dar es Salaam.

Akijieleza juu ya taarifa ya kuitwa kwake na Baraza hilo, Muumini amesema alipigiwa simu na kuelezwa kuwa wimbo wake wa Kwa Mpalange una shida.

“Nilipigiwa simu na kuelezwa kutakiwa kufika Basata na nimeitikia wito lakini kubwa ni wimbo wangu wa Kwa Mpalange, hivyo nitawasikiliza maelekezo watakayonipa maana si unajua Basata ndio mlezi wetu,” amesema Muumini.

Muumini aliongeza kuwa aliandaa na kuachia wimbo huo wa maadhi ya singeli ili kuwapa burudani mashabiki wa muziki wake na singeli kwa ujumla.

Kwa sasa Muumini ambaye aliwahi kutesa na nyimbo mbalimbalii kiwemo Kilio cha Yatima, Mgumba amezaa na Tunda, ameirudisha tena bendi yake ya ‘Tamtam’.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *